
Andriy maykola shevchenko alizaliwa septemba 29, 1976 katika mji wa Dvirkivshchyna nchin Ukraine.
Aprili 1986 akiwa na umri wa miaka tisa sheva na familia yake waliishi maisha ya wakimbizi baada ya kijiji chao kuathiriwa na mionzi ya mabomu ya nyuklia na hivyo kuhamia katika pwani ya mashariki karibu na jiji la Donetsk ili kuepuka madhara ya kemikali za nyuklia.
Baba wa sheva mykola alikuwa ni fundi katika jeshi la ukraine wakati mama yake Lyubov alikuwa ni nesi hivyo kuhama kwao kulitoka na ufahamu wao kwamba jambo lolote baya lingeweza kutokea kwa familia hiyo na nyingine.
Akiwa mdogo sheva pia aliwai kucheza michezo mbalimbali kama ngumi aliolazimika kuuacha kwa kuwa hakuwa na mwili uliojengeka vizuri, pia alishiriki katika mieleka, ice hockey na mpira wa kikapu. Hata hivyo baadaye aliangukia katika soka na kulamba dume, alipoulizwa kulikoni alisema "soka iliupendeza moyo wangu nilichagua soka, soka nayo ikanichagua mimi sikuweza kupenda gofu kwa sababu ukraine hakukuwa na viwanga vya golfu".
AKIWA DYNAMO KIEV
Mwaka 1986 sheva alifeli vibaya mtihani wa soka wa kupiga chenga ambao ungemwezesha kujiunga na shule maalumu ya soka lakini aliendelea kucheza soka akiwa na miaka 13 alijiunga na timu ya vijana wadogo ya Dynamo Kiev baada ya kuvutiwa na kipaji chake.
Ambapo alishiriki katika michuano ya chini ya miaka 14 iliyojulikana ka IAN RUSH CUP {sasa welsh super cup} nchini wales na kuibuka mfungaji bora na kuzawadiwa pair ya viatu na mchezaji wa zamani wa liverpool IAN RUSH
Msimu wa mwaka 1992-92 sheva alikuwa mfungaji bora wa Dynamo akiwa amefunga magoli 12 huku akiwa ameanza kucheza mechi 11.
Na kufanikiwa kunxakua kombe la ligi.
Msimu unaofuatia sheva alifunga magoli sita katika mechi 20 alizocheza.
1998-98 sheva alifanikiwa kufuna hat-trick yake ya kwanza ni katika michuano ya kombe la club bingwa ulaya katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Barcelona.
Pia alifanikiwa kufunga magoli 19 katika mechi 23 za ligi na magoli 6 katika mechi 10 za ligi ya mabingwa ulaya na kumfanya awe amefunga magoli 28 katika michuano yote. Pia alifanikiwa kunyakua ubingwa wa ligi kwa msimu wa tano.
AKIWA AC MILAN.
1999 sheva alijiunga na ac milan kwa uwamisho wa rekodi katika serie a kwa ada ya dola za kimarekani milioni 25.
Alianza kucheza mechi yake ya kwanza agosti 28, 1999 katika mechi ambayo walitoka sare 2-2 na US-Lecce.
Sheva amekuwa mchezaji wa kwanza wa kigeni kuibuka mfungaji bora katika serie A akiwa amefunga magoli 24 katika mechi 32 alizocheza.
Sheva anakuwa mchezaji wa kwanza toka ukraine kutwaa kombe la club bingwa ulaya ni baada ya kuwafunga maasimu wao kwa mikwaju ya penati mwaka 2003 na kuchukua kombe na alikwenda nalo mpaka kwenye kaburi la kocha wake wa zamani Valery Lobanovsky, akidai kwamba ni heshima kwa kocha huyo kwa msaada aliompa hadi kufikia hatua ya kuwa mmoja wa wanasoka bora duniani.
Mwaka 2004 sheva alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa ulaya na kumfanya kuwa mchezaji wa tatu toka ukraine kutwaa tuzo hiyo wengine ni Oley Blokhin na Igor Belanov.
Februari 8, 2006 sheva alikuwa mmchezaji wa pili kwenye club ya Ac milan nyuma ya Gunnar Nordahl kwa goli alilofunga dhidi ya Trevido.
AKIWA CHELSEA.
Sheva alisajiliwa toka ac milan kwa ada ya paundi za uingereza milion 30 na kuvunja rekodi ya Michael Essien.
Alianza kucheza mechi ya kwanza akiwa chelsea august 13, 2006 katika mechi ya kuwania ngao ya hisani na kufanikiwa kufunga goli kwenye mechi ambayo walifungwa 2-1 na liverpool.
Agosti 23 2006 sheva alifunga goli lake la kwanza katika ligi na goli la 300 katika historia yake ya soka katika mechi waliofungwa 2-1 dhidi ya Middlesbrough.
AMERUDI AC MILAN
Agosti 23, 2008 ac milan walitangaza kumsajili sheva toka chelsea kwa ada isiyotangazwa lakini ni dili linalohusu mkopo.
Sheva anakuwa mchezaji wa tatu baada ya Ronaldinho na Flamin kuchagua jezi ilikuwa na namba ya mwaka aliozaliwa 76 ni baada ya kukuta Alexandre Pato kuvaa jezi namba 7.
Agosti 31, 2008 sheva alirudi katika rerie A kwa kuingia kipindi cha pili akipishwa na Merek Jankulovsk katika mechi waliofungwa 2-1 na Bologne.
MECHI ZA KIMATAIFA
Sheva amecheza mechi 82 na kufanikiwa kufunga magoli 36.
Sheva alianza kufunga goli katika timu ya taifa may 1996 katika mechi ya kirafiki dhidi ya Uturuki.
Sheva alifunga magoli 10 katika mechi za kuwania kufuzu kombe la dunia 2002 lakini hawakufuzu ni baada ya kufungwa na Ujerumani.
Alifunga jumla ya magoli matano katika mechi za kufuzu michuano ya ulaya 2008.
MAISHA YAKE BINAFSI.
Sheva amemuoa mwanamitindo wa kimarekani Kristen Pazak walipokutana katika Giorgio Arman mwaka 2002, na kufunga ndoa july 2004 na kufanya sherehe yeke mwenyewe katika uwanja wa golfu huko Washington DC na kuwasiliana na wenzake walio itali.
Sheva alijiuna na chelsea ni kutokana na kuwa na urafiki na mke wa Abromovich pia alitaka watoto wake wawe na utamaduni wa kuongea lugha ya kingereza.
Sheva ana watoto wali Jordan{alimpa jina la mkongwe wa kikapu wa NBA Michael Jordan} aliyezaliwa october 29, 2004 na Christian aliyezaliwa Novemba 10, 2006.
2005 juni alitangazwa kuwa balozi wa watoto wanaoishi kwenye mazimira magumu vijijini.
No comments:
Post a Comment