Tuesday, August 26, 2008

ZINEDINE YAZID ZIDANE "ZIZOU"




MAISHA YA ZIDANEZidane ni malgeria ambaye alizaliwa ufaransa, wazazi wake walikuwa wanakaa katika jimbo la KABYLIE kijiji cha AGUEMONE na kuhamia ufaransa katika jiji la paris mwaka 1953 na baadaye kuhamia MARSEILLE.
Ambapo tarehe 23 june 1972 zidane alizaliwa katika jiji la marseille na kuepewa jina la utani la ZIZOU.
Kiungo huyu wa zamani wa ufaransa alikuwemo kwenye kikosi ambacho kilitwaa ubingwa wa dunia mwaka 1998 na EURO 2000 na kupata mpira wa dhaabu baada ya kuingoza ufaransa katika kombe la dunia mwaka 2006 katika mechi ambayo alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumpiga beki wa italy marco materazzi kichwa.
Amecheza club nne na kutwaa club bingwa ulana akiwa na Real Madrid mwaka 2002.
Ni mmoja kati ya wachezaji wawili kuwa wachezaji bora mara tatu mwinine ni RONALDO DE LIMA
Alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa ulaya mwa 1998.
Mwaka 2004 mashabiki walimchagua kuwa UEFA 15 unnversary golden jubilee pull na ni kujumuishwa na pele katika orodha ya wachezaji 100 bora baada ya kustaafu soka mwaka 2006.
Lakini mwaka june 2008 alifanyiwa mahojiano na BBC na kusema kwamba anatamani kurudi kucheza mpira kwani anashughuli yeyote ya kufanya.

AKIWA CANNES & BORDEAUX 1988-1996
Zidane aliaza kucheza mpira katika timu ya vijana ya us saint henri ambayo ni ya mitaani katika jimbo la La Castellane akiwa na umri wa miaka kumi na nne.
As cannos scout Jean Varraud alimchukua na kujiunga na AS CANNES.
Zidane alianza kucheza ligue 1 akiwa na miaka 17 na alifunga goli lake la kwanza 8 february 1991 na akazawadiwa gari na raisi wa timu kwa msimu wa kwanza kwa kuiwezesa cannes kucheza katika kombe la UEFA.
Zidane aliamia BORDEAUX msimu wa mwaka 1992-93 na kushinda kombe la intertoto na kushika nafasi ya pili katika kombe la UEFA.1995-96
Kwamiaka minne alijenga ushirikiano na BIXENTE LIZARAZU na CHRISTOPHE DUGARY ambaye sasa ni afisamasoko wa Bordeux na mwaka 1998 walikuwa wote kwenye timu ya taifa.
Mwaka 1995 kocha mkuu wa b'burn rovers Kenny Dalgish alimueleza mmiliki wa timu kuwa ana taka kumsajili zidane na dugary mmliki wa timu JACK WALKER alimjibu na kusema kwanini zidane wakati tunaye TIM SHEXWOOD.

JUVENTUS
Mwaka 1996 zidane alihamia kwenye club bingwa ya ulaya juventusfc kwa ada ya £3 million.
Zidane alikuwa mchezaji chaguo la kwanza la kocha marcello Lippi na kunyakuwa ubingwa wa scudetto mwaka 1996-97 na ubingwa wa mabara kwa ushindi wa bao 1-0 walilowafunga river plate.
Nakufanikiwa kufika fainaili ya champions league na juventus na kufungwa goli 3-1 na Borussia Dortmund.
Alifunga goli saba katika mechi 32 alizocheza na kuisaidia juvenus kushika nafasi ya pili katika fainali ya club bingwa kwa kufungwa na real madrid kwa goli 1-0.
Mwaka 2000-01 katika ligi ya serie A juve ilimaliza ikiwa nafasi ya pili nyuma kwa poiti 2 kwa mabingwa AS ROMA.
Zidand alitolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kwa kumpiga kichwa mchezaji wa HAMBURGERSV JACHEN KIENTZ mwaka 2000-01.
Alifanikiwa kufunga magoli 24 kwa muda wote aliocheza juve, alifanikiwa kunyakuwa intercontinental cup 1999 na intertoto cup na makombe mawili ya scudetti.

REAL MADRID 2001-06
Mwaka 2001 zidane alijiunga na real madrid kwa €76 milioni na kufanya kuwa mchezaji ghali kuliko wote katika historia ya soka na alisaini mkataba wa miaka minne.
Mwaka 2002 walifanikiwa kunyakua kombe la club bingwa ulaya kwa kuifunga BAYER LEVERKUSEN kwa magoli 2-1 katika jiji la GLASGOW pia walipata kombe la EUROPEAN SUPER CUP na SPANISH SUPER CUP.
2003 zidane alitajwa kuwa mchezaji bora wa dunia wa fifa wa mwaka na kuungana na RONALDO kwa kuwa wachezaji pekee kuwa wachezaji bora mara tatu.
Alifunga hat-trick katika ushindi wa goli 4-2 dhidi ya sevilla.
Zidane aliishia nusu fainali ya kombe la COPA DEL REY na kumi na sita bora ya club bingwa ulaya, na kumaliza ligi ikiwa nyuma kwa pointi 12 kwa BARCELONA.
7 may 2006 zidane alitangaza kustaafu soka kabla ya kucheza mechi ya mwisho ya nyumbani BERNABEU na kutoka sare ya 3-3 na VILLAREAL CF
Na wachezaji wenzake wakiwa na jersey ikiwa imeandikwa "ZIDANE"2001-06.

SOKA LA KIMATAIFA
Zidane alikuwa ni raia wa ufaransa na algeria yeye alipenda kucheza timu ya taifa ya algeria lakini kocha ABDELHAMID KERMALI akumtaka kwenye kikosi chake akidai bado mdogo sana na katika nafasi ya kiungo.
Mwaka 2005 zidane alipinga uvumi wa kuwa awezi kuchezea timu ya taifa ya algeria kwakuwa ameipenda ufaransa.
Mwaka 1998 zidane aliweza kuiongoza ufaransa vizuri na kufanikiwa kutwaa kombe la dunia kwa kuitandika brazil kwa magoli 3-0.
Mwaka 2000 aliiwezesha ufaransa kutwaa kombe la ulaya kwa kuifunga italy
Mwaka 2002 zidane akucheza mechi mbili za makundi katika michuano ya kombe la dunia kwa kuwa majeruhi lakini alicheza mechi ya tatu na kufanya kutolewa katika hatua ya makundi wakiwa hawajafunga goli hata moja.
Mwaka 2006 aliisaidia ufaransa kufika fainali ya kombe la dunia lakini alitolewa nje kwa kadi nyekundu katika dakika ya 110 kwa kumpiga kichwa beki wa italy MARCO MATERAZZI.
Alifunga goli kwa mkwaju wa penati na kumfanya awe mmoja wa wachezaji wanne kufunga katika fainali mbili tofauti wengine ni PELE,VAVA na PAULO BREITNER na PELE VAVA na GEOFT HURST ni wachezaji waliofunga magoli matatu katika fainali za kombe la dunia.

UGOMVI NA MARCO MATERAZZI
Zidane na beki wa italy marco materezzi walikuwa wanaongozana uwanjani lakini zidane alisimama na kumpiga kichwa cha kifua lakini refaree HARACIO EIZONDO akumuona mpaka pale alipopewa taarifa na kamisaa LUIS MEDINA na kupewa kadi nyekundu katika dakika ya 110.

No comments: