

Pele alizaliwa october 23 1940 huko TRES CORACOES BRAZIL.
Anaurefu wa 1.74m{5ft0.5in}
Alizaliwa na JOAO RAMOS DO NASCIENT mchezaji wa zamani wa FLUMINENSE aliyejulikana kama DENDINHO na MARIA CELESTE ARANTES walimpa jina la inventor wa kimarekani THOMAS EDISON na jina lake la utani alijulikana kama DICO katika familia yake.
Alipata jina la utani la PELE akiwa anasoma shule. Pele aliitwa kutokana na makosa ya kimatamshi lililotokana na jina la golikipa wa zamani wa vasco da gama "BILE" na kulibadilisha na kuitwa "PILE" jina ambalo akulipenda.
Pele alisimamishwa shule kwa kumpiga mwanafunzi mwenzake kwa kumwita jina hilo.
BILE walilipeleka kwenye lugha ya ki irishi na likasomeka PEILE likimaanisha FOOTBAL.
Pele alikulia kwenye maisha ya kimaskini huko Baura Sáo Paulo.
Alijipatia fedha kwa kubrashi viatu vya club ya Baura Athletic kwenye siku za mechi.
Pele alianzakutengeneza mpira wa makaratasi ya magazeti na kamba na kuweka soksi au matunda yaliyokaa kama mpira.
Mwaka 1954 vilabu vya america vilimtamani pele ambaye alijiunga na timu ya Baquinho boys timu ambayo ilikuwa inanolewa na mchezaji wa zamani wa kimataifa wa brazil WALDEMAR DE BRITO ambaye alishiriki kwenye kombe la dunia mwaka 1934 huko italy.
AKIWA SANTOS
Mwaka 1956 DE BRITO alimchukua pele na kumpeleka santos huko sao paul kujaribu soka la kulipwa na club ya santos futebol clube.
Akiwa na miaka 15 alikuwa mchezaji mkubwa duniani.
Akiwa santos pele alifanikiwa kucheza na wachezaji wakubwa sana duniani kama zito pele na coutinho ambao alicheza nao moja mbila na kufunga magoli.
Pele alifanikiwa kufunga goli lake la kwanza akiwa na jezi ya santos tarehe 7 september 1956 katika ushindi wa goli 7-1 katika mechi ya kirafiki dhidi ya Corinthians.
Wakati unaanza mwaka 1957 pele alianza katika timu ya kwanza akiwa na umri wa miaka 16 na kuwa mfungaji bora katika ligi miezi kumi baada ya kusaini mkataba.
Kocha mkuu wa timu ya taifa alimwita kwenye timu ya taifa ya brazil.
Baada ya fainali za kombe la dunia za mwaka 1962 vilabu vikubwa ya ulaya vilitoa ofa ya kumsajili kijana huyu lakini selikari ya brazil ilikataa na kusema pele ni kivutio cha taifa kwahiyo awezi kuondoka nchini mwake.
Nov 19, 1969 pele alifunga goli lake la elfu moja 1000 katika michuano yote ilikuwa dhidi ya vasco da gama kwa njia ya penati katika uwanja wa Maracana na kulidedicate kwa watoto wote wanaoishi kwenye maisha ya kimaskini nchini brazil.
Pele alifunga goli zuri katika uwanja wa compeonato paulistu ilikuwa mechi dhidi ya sao paulo 2, august 1959. Kulikuwa hakuna video iliyochukua mechi hiyo ambayo ilishindwa kuwekwa kwenye computer.
March 1961 pele alifunga goli lililojulikana ka "goal of plague" ilikuwa dhidi ya fluminese katika uwanja wa wa Maracana na kulifanya kuwa goli zuri kuliko yote yaliyo wahi kutokea katika uwanja wa MARACANA.
1967 huko nigeria walisimamisha vita ya wenyewe kwa wenyewe kwa masaa 48 kwa kumuangalia pele katika mchezo uliofanyika lagos.
NEW YORK COSMOS
Baada ya msimu wa mwaka 1972 akiwa na santos pele alistafu katika club hiyo ya brazil baada ya miaka miwili baadaye pele alijiunga ya New york cosmos ya amerika kaskazini soccer league {NASL} akiwa marekani pele aliweza kufunga magoli ya ticktack au bicycle kick na kusababisha watu wengi wafungulie kituo cha tv cha michezo cha sports tv series, ABC'S wide world of sport.
Oct.1.1977 pele alicheza mechi yake ya mwisho ya kumuaga kati ya cosmos na santos. Santos walikuja New york na New jersey na kuibuka na ushindi wa goli 2-0 mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Giants na kurushwa na kituo cha television cha ABC'S wide world of sports na kuonekana kote duniani.
Baba na mke wake waliudhurha mechi hii.
Kabla ya mechi pele aliutubia na kusena "LOVE" mara tatu.
Kipindi cha kwanza pele alicheza timu ya cosmos na kipindi cha pili alicheza santos.
Reynaldo alifunga goli la kwanza baada ya kumalizia cross.
Pele alifunga goli la pili kwa njia ya adhabu.
Katika kipindi cha mapumziko pele alivua shirt no 10 na kumpelekea baba yake alisindikizwa na mchezaji mwenzake wa cosmos Ramon Mittlin ambaye alimbadili pele ambaye alifunga goli na kufanya matokeo yawe2-1 na baada ya mechi pele alishika bendela ya marekani mkono wa kulia na bendela ya brazil mkono wa kushoto.
Wakati anacheza mpira alijulikana kam MFALME WA MPIRA{o rei do futebol} MFALME PELE {o rei pele}
Aliitwa kwenye timu ya taifa akiwa na umri wa miaka 16 na kunyakua kombe la dunia akiwa na umri wa miaka 17.
Muda wote aliokuwa anacheza pele alikuwa mfungaji bora katika timu ya taifa ya brazil.
Na ni mchezaji pekee kushinda makombe matatu ya kombe la dunia.
Mwaka 1962 alijumuishwa kwenye kikosi cha brazil na alipata majeruhi na kufanya asipewe medali.
Nov 2007 FIFA walitangaza kwamba anastahili kupata medali ya mwaka 1962. Na kumfanya awe mchezaji peke kutwaa medali ya kombe la dunia.
Tangu amestaafu 1977 pele amekuwa balozi wa mpira katika FIFA na kivutio cha serikali ya brazil.
Pia alichaguliwa kuwa mchezaji wa karne na kupewa tuzo na international olympic committee.
No comments:
Post a Comment